HEADLINES

6/recent/ticker-posts


FUNDO LA MWISHO


MJUE JELLY FISH SAMAKI HATARI ZAIDI DUNIANI

Na AMEDEUS SOMI, DSM


Bonjue bila shaka wewe ni mzima wa afya na siku zinasonga mno kwako, kama jibu ni ndio basi vuta kiti kaa kwa kutulia menu inakuja muda sio mrefu ikibidi washtue wenzio kabisa.


Dunia ina mengi, na ukistaajabu ya Mussa utayaona ya mzee Mpili wa Ikwiriri aliyetrend na Wazee wa Jangwani kwa muda mfupi Zaidi kuwahi kutokea, ukiniuliza sasa hivi yuko wapi sina jibu, tushkilie hapo hapo.


Najua umewahi kusikia viumbe wakali,wenye nguvu au wenye sumu kali zaidi duniani, Najua pia umewahimsikia nyoka aina ya  Koboko au Black Mamba ambaye anasifika kwa kuwa na sumu kali zaidi ulimwenguni lakini mzee unaambiwa hafurukuti mbele ya Jelly Fish.


Sasa banja kwanza weka koo vizuri alafu twende sawa au vuta kimfuko chako cha popcorn anza kushushia na FUNDO LA MWISHO akili ikae sawa incase kama nimekuacha popcorn kwa kiswahili zinaitwa bisi..najua hapa watoto wa kiambankule hawawezi nielewa.


Jelly Fish ndio Samaki hatari zaidi  Ulimwenguni, najua wavuvi wa Mafia au Rufiji wanaweza wasimfahamu wakiamini Mkizi ndio balaa nop.kumbe kuna Kidubwasha kidogo tu kinachosumbua akili za wavuvi tena wazungu katika bahari ya Pacific.


Jelly Fish ni samaki anayepatikana  baharini, hasa katika bahari ya Pacific na Atlantic. Samaki huyu hupatikana kwa wingi katika nchi za Australia, New Zealand,Ufilipino na Mji wa Hawaii uliopo nchini Marekani.


Samaki huyu hujulikana kama “the most deadliest fish in the world”the most venomous creature na “the most notoriously dangerous specie in the world yaani kiumbe hatari zaidi hapa chini ya jua.


Jelly Fish kwa Lugha ya Kijapani wanajulikana kama “Kurage”au “Japanese Jelly Fish” 


Kwa viumbe wa ardhini na majini tunaweza kupima ukali wake wa kuua kwa sumu kwa kuangalia vigezo viwili.


Sumu yake anayotoa kwa kipimo cha ounce yaani (ounc 1=28.3 gram)ina uwezo wa kuua watu 60 kwa mpigo tena chini ya dakika 3 tu.


Kwa kutumia vigezo hivyo utaona kuwa Jelly Fish anawazidi makilomita viumbe wengine wote wa baharini na nchi kavu kwa kuwa na sumu kali yenye kuweza kuua watu wengi na kwa haraka mno.



SUMU HUSHAMBULIA NINI MWILINI MWA MTU?


Kama akikupiga na sumu yake inaenda kwa haraka kushambulia moyo na kuua mifumo ya nerva ya neva hivyo kupelekea kufa kwaharaka Zaidi.



KITU GANI NI HATARI ZAIDI KWAKE?


Kuna kamsemo kanasemaga unaweza kuwa mkali kwenu lakini ukija kwetu unaweza ukawa kit manager yaani mbeba vifaa tu wakati wakali wanaenda ulingoni.

Samaki huyu hafurukuti wala hachomoi kwa Samaki Kasa kwa sababu sumu yao haimdhuru nadhanini kulingana na lile gamba gumu walilonalo kama mzigo wa shida ndio linawasidia.


JE SAMAKI HUYU ANAFANANAJE?


Jelly Fish ukimtazama kwa umbo lake unaweza kusema ni kiumbe dhaifu na hata cha kufuga ili ukichezee maana yupo ama maua.Kwa wale walioangalia movie ya Pound ya Wily Smith watakuwa wamemuona pale mwishoni.



Maisha ya Jelly Fish ni kama ifuatavyo ukumbwa wake unakuwa na urefu wa cm 20,miguu yake inakuwa na urefu wa kufikia mita 3 huku akiwa na uzito wa kilo 2, Jelly Fish ana jumla ya macho 24 ambayo yamekusanyika 6 katika kona nne za mwili wake, wanaishi kwa muda wa mwaka 1 tu toka wazaliwe.



ANAULIWAJE?


Wahenga wanasema dudu liumalo usilipe kidole kama ingekuwa ni hapa bongo aisee wapemba wangeshamtaftia namna ya kumsepesha maana angewaletea usiku kwenye shughuli zao za Pwani.


Inaelezwa mpaka sasa hakuna binadamu aliyefanikiwa kumuua samaki huyu maana kila unapokata miguu yake huchipua kama majani, ni kiumbe cha ajabu pia ambacho hata binadamu na akili zao wameshindwa kumuua.


Shukrani za dhati ziwaendee taasisiya utafiti wa viumbe wa majini ya IUCN Eastern Africa Programme kwa kunipaushirikiano katika kuandaa Makala hii uwe na siku njema.



Kwa Habari na matukio ya kushangaza Unaweza kunifata katika ukurasa wangu wa Instagram natumia

  @officialsomithegreat 


Gusa Link Kwenda Kutazama 👇👇





Post a Comment

0 Comments