HEADLINES

6/recent/ticker-posts

Serikali Imepongeza Maendeleo ya Mradi wa FISH4ACP Ziwa Tanganyika

 Serikali Imepongeza Maendeleo ya Mradi wa FISH4ACP Ziwa Tanganyika



Na Mwandishi Wetu


Serikali imetoa pongezi kwa wachambuzi wa mnyororo wa thamani kwa kazi  ya kuboresha uchambuzi wa mnyoro wa thamani huku ikisifia mradi wa FISH4ACP .


Akizungumza mjini  Kigima katika Warsha juu ya kukuza mnyoro huo katika  dagaa na mgebuka wa Ziwa Tanganyika nchini , Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi  amesema kuwa lengo ni kuwa na ustawi wa kiuchumi na uzalishaji wa ajira kwa  kuhakikisha uendelevu kiuchumi na kijamii.


"Mijadala umezingatia kupata mpango bora utakao tekelezeka ili kuchangia ajira pana pamoja na malengo ya kitaifa na kimataifa,"amesema Rashid  .


Amesema katika kipindi cha mwaka huu 2021 Benki ya NMB tayari imeanza kuvitambua vikundi vyenye uitaji ili kuweza kuvikopesha .


Pichani Wavuvi wa Ziwa Tanganyika juzi asubuhi wakiwa katika harakati zao  za uvuvi katika Mwalo wa Katonga Mkoani Kigoma.


Katika mchakato huo mpana juu ya kukuza mnyororo huo wa thamani wa Ziwa Tanganyika Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)  Dkt. Ismaili Kimirei amesema FISH4ACP wamekuwa wadau katika mpango wa utekelezaji wa mkakati wa maboresho  2021 - 2024 .


"Mradi wa FISH4ACP ambao umekuwa utekelezwa kwenye nchi 12 unafadhiliwana umoja wa ulaya (EU) na serikali ya ujerumani unagjarimu kiasi Cha Euro milioni tati,"amesema Dkt.Kimirei.


Mvuvi katika Mwalo wa Katonga Francis John yeye amesema kuwa mradi huo utawezesha kukua kwa soko la samaki katika ziwa hilo ambapo tayari samaki wake  kwa soko la nje , nchi za Australia na Marekani wamekuwa ni wateja katika soko

Post a Comment

0 Comments