HEADLINES

6/recent/ticker-posts

AUGUSTINO MREMA AFARIKI DUNIA ASUBUHI HII




Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam

 Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki duninia leo Jumapili, Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.  Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo. 

Enzi za uhai wake, Mwanasiasa huyo aliwahi kuwa Mgombea Urais kupitia NCCR-Mageuzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na Chama hicho akitokea CCM

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na umauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Post a Comment

0 Comments