HEADLINES

6/recent/ticker-posts

DC KIGAMBONI AFANYA ZIARA KUFATILIA ZOEZI LA SENSA


Na Amedeus Somi,

Dar es Salaam,



Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almasi Nyangasa amefanya ziara ya kufuatilia mwenendo wa zoezi la sensa katika kata mbalimbali za wilaya ya Kigamboni

Nyangasa amesema zoezi hilo linaendelea vizuri na mpaka sasa limefikia kwa watu wengi zaidi

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewaasa wananchi kuendelea kujitokeza na kutoa ushirikiano

"Zoezi linaendelea vizuri na wananchi watoe ushirikiano, tupo vizuri na kila mmoja lazima atahesabiwa"


Zilizosomwa

 

Hata hivyo Mratibu wa Sensa wilaya ya Kigamboni Railu Ramadhani Ngonya amesema

"Zoezi kwa Kigamboni linaenda vizuri na lilianza usiku wa kuamkia tarehe 23 ambapo zilihojiwa kaya maalum na mpaka sasa kuna baadhi ya maeneo makarani wameshamaliza kama Ferry, kinachofanyika ni kupeleka makarani katika maeneo mengine"


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatuma Nyangassa akitoa maelekezo kwa viongozi na makarani wa Sensa katika Mtaa wa Uvumba

 

Ameongeza kuwa changamoto wanazokutana nazo ni kwa zile kaya ambazo wakazi wake wanatoka asubuhi kwenda kwenye shughuli za utafutaji na kurudi jioni.

Ametoa wito kwa wananchi kujaza kwa usahihi karatasi za Sensa wanazowaachia

Wananchi waliohesabiwa pia hawakuwa nyuma kwani walikuwa na haya ya kusema mara baada ya kuhesabiwa



Post a Comment

0 Comments