HEADLINES

6/recent/ticker-posts

DR ABBAS AKUMBUSHA WAANDISHI WAJIBU WAO, TIMU ZA TAIFA HAZINA NJAA

Na Amedeus Somi

DAR ES SALAAM,



 Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amewahimiza Wanahabari za michezo kulinda hadhi ya taaluma yao ya habari kwa kufuata misingi yake, kwani hiyo ni kazi ya kikatiba na yenye umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu na nchi kwa ujumla.


Dkt. Abbasi amezungumza hayo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari za michezo iliyofanyika leo Agosti 29, 2022 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la NSSF (Mafao House), Ilala mkoani Dar es Salaam.

"Waandishi kazi mnayoifanya ni kwa kubwa sana ukitoa Serikali Bunge na Mahakama mnafata ninyi, Mwandishi ana majukumu ya kufanya ugunduzi wa mambo na kuyapatia ufumbuzi mfano kama Ugonjwa wa Uviko. Waweza kutafuta nini chanzo nini kifanyike ili kuleta msaada"

"Mwandishi  ni Daraja kati ya Wananchi na Viongozi, mfano wa kijinsia wasomi na walemavu"


Aidha Dr. Abbas amezungumzia mamo mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya Tanzania kama vile garama zinazotolewa na Serikali kwa Timu za Taifa za Michezo mbalimbali

Dr. abass amedndelea kusema kuwa ni gharama kubwa kupeleka timu  moja ya mchezo mmoja kwa mechi moja nje ya nchi akisema inagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Millioni 300 mpaka 400.


Amtaja Rais Samia kama mtu wa kazi kwa kubuni vyanzo vya fedha za michezo asilimia tano kutoka katika Makampuni ya kubashiri.Akisisitiza kuwa Wizara inajenga ushawishi wa kupata fedha kutoka Serikalini kama vile kwasasa asilimia 2 ya fedha kutolewa serikalini kwenda kwenye michezo.

 Dr. Hassan Abbas ameendelea kusema kuwa serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi Billion mbili  kwa ajili ya kambi za maandalizi za timu za Taifa huku akisema hii haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Wizara hiyo.

"Serengeti Girls itakwenda kupiga kambi ya maandalizi nchini Uingereza katika Klabu ya Southampton ikipata mechi za kirafiki pamoja na timu nyingine za wanawake za hapo Uingereza.

"Baada ya hapo itaelekea katika nchi za Kiarabu kabla ya kwenda India kwenye Kombe la Dunia "  


Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, amesema matunda yaliyopatikana kwenye Olimpiki ya mwaka huu pale Birmingham ni jitihada za serikali kuamua kuwekeza na kujitoa katika michezo.





Post a Comment

0 Comments