HEADLINES

6/recent/ticker-posts

ALICHOKISEMA MHE. BARAKA LUVANDA BALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUPITIA MTANDAO


Na Mwandishi wetu

"Kumbukumbu zinaonyesha kuwa misaada ya Japan kwa Afrika imeongezeka kutoka Dola la kimarekani Milioni 0.6 kwa mwaka 1993 hadi Dola za Kimarekani Milioni 20 mwaka 2009"

"Licha ya changamoto zilizopo wakati huu kama vile janga la Uviko, vita kati ya Ukraine na Urusi, Mabadiliko ya tabianchi Serikali ya Japan bado imetoa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 30 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2022 mpaka 2025 kwa nchi za Afrika Ili kuziwezesha kutekeleza programu na miradi ya maendeleo itakayochochea mageuzi ya kiuchumi"

"Kwa kuhakikisha kuwa matumizi ya nishati ya salama na rafiki kwa Mazingira Japan itazindua Mpango wake wa Japan's Green Growth initiative with Africa na kutoa Dola za kimarekani Milioni 4 za kutekeleza mpango huo kupitia vyanzo vya serikali na sekta binafsi"

"Japan kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika itafadhili kiasi kinachofikia Dola za kimarekani Bilioni 5 kwa ajili ya kuboresha ustawi wa maisha ya watu wa Afrika hii itahusisha mikopo mipya ambayo itafikia Dola za kimarekani Milioni 1 kwa lengo la kuleta mageuzi na matokeo chanya kwenye usimamizi na Udhibiti endelevu wa madeni Barani Afrika"

" Japan imetoa kiasi kinachofikia Dola za kimarekani Bilioni 1.08 kupitia Global Fund ili  kupambana na Uviko ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo, huu ni Mkakati ambao serikali ya Japan inaichangia Afrika katika dhana ya Usalama wa binadamu ikiwa ni jukumu lake la msingi"

"Mpango wa kuhamasisha Maendeleo ya rasilimali watu barani Afrika kwa kuwajengea uwezo vijana wa Afrika kwenye sekta ya viwanda, afya, elimu, kilimo, sheria, na utawala inakadiriwa vijana zaidi ya laki tatu watanufaika na Mpango huo"

"Japan imeahidi kuendelea kufanya mapitio ya sheria zake za masuala ya usafiri iliyotokana na tahadhari ya magonjwa ya kuambukiza hususani Uviko kutoka nchi za Afrika ili kutanua wigo wa muingiliano wa shughuli na watu kati ya Japan na Afrika, kulegezwa kwa masharti hayo kutawezesha programu za mafunzo yaliyokuwa yamesitishwa kufanyika ana kwa ana nchini humo kuanza tena na tayari makundi mbalimbali ya Tanzania yataanza kuingia Japan kuanzia Septemba na Oktoba mwaka huu"

"Japan itaendelea kusaidia kuimarisha amani barani Afrika ili iweze kutelekeza rasilimali zake katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia wakimbizi walio kwenye kambi mbalimbali katika nchi hizo ili waweze kujikwamua kimaisha, kujitegemea na kuendesha maisha yao wenyewe"

"Na pia Japan  itamteua mjumbe maalum katika pembe ya Afrika kwajili ya kusimamia masuala ya Usalama na amani katika eneo hilo"

"Japan kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika imetoa kiasi kinachofikia Dola za kimarekani Milioni 300 kwaajili ya kuendeleza kilimo Barani Afrika pamoja na kusaidia Mpango wa kujengewa uwezo watu laki mbili kwenye sekta ya Kilimo kwaajili ya kuimarisha Usalama wa chakula"

"Kupitia mpango wa maendeleo ya kilimo barani Afrika Serikali ya Japan imeahidi kuisaidia Tanzania Dola za Kimarekani laki tano kwa ajili ya kununua chakula kwa lengo la kukabiliana na baa la njaa nchini kufuatia athari za Uviko na vita kati ya Ukraine na Urusi"

"Tanzania imechaguliwa kuwa Nchi ya mfano miongoni mwa nchi za Afrika na Shirika la kimaendeleo la Japan JAICA katika mpango wake kuimarisha kilimo Cha uzalishaji wa mpunga Barani Afrika"

"Japan imekubali ombi la Tanzania la kuongeza Uwekezaji wake nchini pamoja na shughuli za kibiashara hivyo viongozi hao wamekubaliana kupitia Balozi zilizopo Dar es salaam na Tokyo kufanya ufatuliaji wa karibu Kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yana fursa za Uwekezaji wa kibiashara"

"Japan imeishukuru Tanzania kwa kufanyia marekebisho  sheria za kodi ambayo imewezesha kusainiwa kwa miradi mitatu ya Arusha Holili ule wa Kigoma na Zanzibar ambao utekelezaji wake umeanza"

"Japan imeiomba Tanzania kushirikiana katika kupaza sauti na kuzikemea nchi ambazo zinatumia nguvu zao za kiuchumi na fedha kuzinyonya nchi masikini na zile zinazoendelea"

Post a Comment

0 Comments