HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MADEREVA BODA-BODA MARA WAANDAMANA MPAKA KWA RPC

NA MWANDISHI WETU
Leo hii madereva bodaboda zaidi ya 100 waandamana mpaka ofisi za mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kwa lengo la kuonyesha kufurahishwa na kitendo cha askari polisi kuwadhibiti majambazi kadhaa wa kutumia silaha mkoani humo. Madereva hao katika tamko lao lililosomwa na afisa habari wa umoja wa madereva bodaboda mkoani humo Bw. Faustine Mbaruku wamelitaka Jeshi la Polisi nchini kuendelea na udhibiti wa uhalifu maana imeleta amani na kuongeza ari ya ufanyaji kazi kwa bodaboda wote mkoani humo. "Nani asiyejua kwa kipindi cha hivi karibuni hakuna kijana wa bodaboda aliyekua anajua kesho ataamka akiwa hai au ataamka akiwa hana jeraha katika mwili wake au akiamka akiwa na bodaboda yake, hali hii ilitupelekea kuteteresha ustawi wa familia zetu" Nae Mwenyekiti wa Boda Boda Mkoa wa Mara ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mikasa ya ujambazi na uhalifu wa silaha za moto ambayo wananchi wa mkoa huo wamekutana nayo haswa madereva boda boda wenzake. "Tunataka bodaboda mkoa wa Mara tuishi salama na familia zetu zibaki salama, kuna matukio ya kutekwa kwa bodaboda na tunaomba Jeshi la Polisi tuendelee kuwasiliana ili kuimarisha zaidi hali ya usalama wetu, ikiwa kuna mtu amekuja kwa ajili ya kufanya uhalifu ni kheri asiwepo miongoni mwetu". Pamoja na hayo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP. Longinus Alexander Tibishubwamu aliwapokea bodaboda hao na kisha kuwapongeza kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa Jeshi la Polisi katika kudhibiti na kufichua wahalifu mkoani humo na kusisitizs kuendelea na majukumu ya msingi ya ulinzi wa raia na mali zao. "Niwahakikishie kuwa sisi tuko pamoja na nyinyi, tunatambua shughuli zenu za usafirishaji katika uje zi wa Taifa, hivyo tunawahakikishia kwamba mtaendelea kufanya kazi masaa 24, mawasiliano yetu mnayo hivyo kunapotokea viashiria vyovyote vya uhalifu msisite kutufahamisha na tutafika haraka kudhibiti hali hiyo"

Post a Comment

0 Comments