HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MAREKEBISHO YALIYOFANYWA NA SERIKALI JUU YA SHERIA YA MIAMALA YA KIELETRONIKI

Waziri wa fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba amesimama Bungeni leo September 20, 2022 na kutoa kauli ya Serikali kuhusu tozo ambapo ameeleza marekebisho yatakayofanyika na kuanza kutumika kuanzia October 1, 2022. Marekebisho aliyoyataja ni pamoja na kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa Benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000 Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala. 1. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote). 2. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja. 3. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine. 4. Wafanyabiashara wadogo hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa. 5. Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000. 6. Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala. Ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000.

Post a Comment

0 Comments