HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TANZANIA NA ZIMBABWE ZAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO SARPCCO


 Na Mwandishi wetu 

DAR ES SALAAM

Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO Games 2022) imeanza katika Uwanja wa Benjemin Mkapa Dar es Salaam  leo tarehe 4 Septemba ambapo  mashindano ya riadha mbio ndefu, fupi na kurusha tufe yamefanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha Interpol Tanzania SACP. Gemini Mushy ambaye ni Katibu wa Kamati ya maandalizi ya michezo ya SARPCCO Games 2022 msimu wa 11  amesema mashindano haya yameanza kuleta mafanikio kwa kutimiza malengo ya kuwakutanisha  askari wa nchi Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kupitia michezo. 

SACP Mushy, amewataka wananchi kujitokeza  viwanjani kuweza kutizama michezo pia kuwashangilia wachezaji wao wa Jeshi la Polisi ambao wanashiriki mashindano haya.

Katika michezo iliyofanyika leo kwa mbio ndefu mita 10000 kwa wanaume zimekamilika ambapo mshiriki kutoka  Zimbabwe amechukua medali ya dhahabu akifuatiwa na mshiriki wa Tanzania na katika mbio za mita 5000 wanawake  mshiriki wa Tanzania  Asha Salum amechukua medali ya dhababu akifuatiwa na  Mshiriki kutoka Zimbabwe




Post a Comment

0 Comments