HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WANUNUZI WA TUMBAKU AMBAO HAWAJAWALIPA WAKULIMA WACHUKULIWE HATUA - MAJALIWA

Na Mwandishi wetu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza wanunuzi wote ambao wamechukua tumbaku za wakulima na hawajawalipa fedha zao wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kwani Serikali inataka kuona wakulima wakinufaika na zao hilo. “Tumbaku katika mkoa wa Tabora ni uchumi, hivyo viongozi kuanzia ngazi ya wizara, mkoa, wilaya, kata na hata vijiji simamieni ushirika kwenye maeneo yenu, ushirika ni uchumi. Sote tuwajibike kwa pamoja, tuhakikishe ushirika unapata mafanikio.” Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Septemba 9, 2022) wakati akizungumza na viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika, AMCOS na wakulima wa tumbaku kutoka wilaya za Urambo na Kaliua, mkoani Tabora. Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan haitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kuhujumu ushirika nchini kwa sababu imedhamiria kuuboresha.

Post a Comment

0 Comments