HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MAADHIMISHO SIKU YA MBOLEA DUNIANI KUFANYIKA SONGWE OKTOBA HII

 



Na Amedeus Somi

DAR ES SALAAM


Maadhimisho ya siku ya Mbolea duniani ambayo hufanyika kila mwaka  tarehe 13 ya kila mwaka yanatarajiwa kufanyika katika Mkoa wa Songwe.

Maadhimisho hayo ni kumbukizi ya uvumbuzi wa kairutubisho cha Naitrojeni kinachopatikana hewani. Uvumbuzi huu ulifanywa na Bwana Fritz Haber mwaka 1908 raia wa Uingereza 

Siku ya mbolea duniani iliadhimishwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 2016 nhini Uingereza.Maadhimisho ya siku hii ni mpango wa Kimataifa unaoungwa mkono na kuelimisha umma hasa wakulima kuhusu faida na matumizi sahihi ya mbolea na kutia moyo juhudi za ubunifu katika teknolojia ya kilimo

Uvumbuzi huu ulichochea mapinduzi ya kijani katika karne ya 20 yaliyowezesha kuongezeka kwa tija katika uzalishaji wa mazao kutokana na matumizi ya mbolea na hivyo kuchangia kupunguza kwa iasi kikubwa janga la njaa na kuleta uhakika wa chakula katika nchi nyingi duniani.

Akizungumza katika mkutano na Wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya Mbolea Tanzania  Dkt Stefan Ngailo amesema maadhimisho hayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 11 Octoba 2022 na kufikia kilele chake tarehe 13 Octoba, 2022 katika viwanja vya Kimondo, Mlowo katika Halmashauri ya Mbozi Mkoa wa Songwe. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe (MB)


Aidha amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mbolea duniani ni kupanua wigo zaidi ya kuelezea masual mbalimbali katika tasnia ya mbolea ikiwemo mafanikio ya tasnia ya mbolea nchini, kutoa elimu kwa wadau wa mbolea hususan wakulima na wafanyabiashara wa mbolea.

Kaulimbiu ya  Siku ya Mbolea Duniani kwa mwak 2022 ni  Ajenda 10/30. Matumizi sahihi ya mbolea ya Ruzuku kwa Kilimo chenye tija.

Post a Comment

0 Comments