HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MWAKIBETE AWAATAKA AQRB KUONGEZA WATAALAM WA MAJENGO

Na Amedeus Somi DAR ES SALAAM Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete, amezungumzia umuhimu wa Bodi ya Usajili Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kuongeza idadi ya wataalam wa fani hiyo waliosajiliwa nchini.   Akifungua mkutano mkuu wa tatu wa AQRB jijini Dar es Salaam Mhe. Mwakibete amesema Serikali itaendelea kutoa ufadhili wa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa fani hiyo kila mwaka ili kuongeza idadi ya wataalamu hao wenye sifa nchini na hivyo kuwawezesha kufanyakazi ndani na nje ya nchi.  
" Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwa uchumi na maendeleo ya nchi hivyo simamieni kikamilifu sekta ya majenzi ili kuboresha miji na kuleta usalama wa majengo," 
"Nimeambiwa kwa sasa Serikali ina wataalamu 9 tu ni jambo ambalo linaketa ugumu kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya serikali kama vile SGR" Mkutano huo unaoongozwa na mada kuu inayosema "uhifadhi wa majengo kwenye miji ya Afrika kwa sasa" unahudhuriwa na wataalamu mbalimbali katika sekta ya ujenzi kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu za kuhakikisha ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi unakwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.   Mwakibete amewahakikishia wataalam hao kuwa  Serikali itaendelea kutoa ufadhili huo ili kuongeza idadi ya wataalamu wazawa  na kuwa katika mwaka  wa fedha 2022/23 Wizara imeidhinisha kiasi cha Shilingi milioni 550 kwa ajili ya Mpango wa Mafunzo ya Wahitimu kwa Vitendo (EAPP).   Naibu Waziri Mwakibete ametoa wito kwa Bodi hiyo kuziangalia upya gharama za usajili wa wanachama ili ziwe nafuu na hivyo kuwawezesha  wataalam wenye sifa kusajiliwa na kuwawazesha wananchi kutumia huduma za wataalam waliosajiliwa.    Mwakibete amesema kuanzia sasa wataalamu wote watahusishwa katika miradi ya ujenzi na kwamba wizara yake imeunda timu maalumu kwa ajili ya kupitia miradi inayoendelea na kutathmini mahitaji yanayotakiwa. Aidha Mwakibete ameongeza na kusema kuwa  
"Kuanzia sasa lazima wataalamu wote washirikishwe kwenye miradi, Serikali itatumia wataalamu katika sekta zote ili kukidhi mahitaji ya makundi yote," amesema Mwakibete.

Post a Comment

0 Comments