HEADLINES

6/recent/ticker-posts





Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Phillip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Tanzania yanayojulikana kama Swahili International Tourism Expo (SITE) kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam, ambapo yatafanyika kwa siku tatu, Oktoba 21 hadi 23 likibeba kauli mbiu ya ‘Kuupeleka Utalii katika Ngazi za Juu (Taking Toursim to the New Heights). 

 Awali akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya maandalizi ya onesho hilo la Sita (6), kwa mwaka huu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Felix John ambaye aliambatana na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mh. Kheri James alisema kuwa maandilizi yote yamekamilika na wadau mbalimbali watahudhuria wa ndani na nje huku likitarajiwa kuleta matokeo chanya katika kukuza Utalii wa Tanzania.   


‘’SiTE 2022 ambalo tumekuwa tukilisubiria kwa hamu kubwa, tangu kuahirishwa kwake onesho la mwisho mwaka2019, tunaamini mchango mkubwa wa Vyombo vya habari na mmekuwa mabalozi wetu wazuri katika kuhabarisha na kutangaza vivutio vilivyopo nchini,   Tayari maandalizi makubwa kabisa kwa kuanza hapo kesho Oktoba 21, Wafanyabishara wa kutoka ndani na nje ya nchi watahudhuria ambapo watapata fursa za kionesha bidhaa, kutengeneza mtandao wa biashara, kuanzisha na kuimarisha mahusiano ya kibiashara’’ alisema Bw. Felix John.  

 Aidha, amebainisha kuwa, tangu kuanzishwa kwake limekuwa la mafanikio makubwa ikiwemo ongezeko la waoneshaji (Exhibitors), na wanunuzi wa kimataifa, hata hivyo lilisimama kwa muda kutokana na mlipuko wa UVIKO 19.  

 ‘’Tutakuwa na mikutano ya wafanyabiashara B2B, B2G, Lakini pia kutakuwa na siku tano (5) za ziara za mafunzo (FAM trips) ambapo watatembelea vivutio vya Utalii nchini ikiwemo Hifadhi za Taifa Serengeti, Mkomazi, Mikumi,Nyerere, Udzungwa   Pia eneo la Ngorongoro, Kisiwa cha Zanzibar na maeneo mengine mbalimbali ya Utalii na Utamaduni.’’ 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Bw. Felix John (katikati) akizungumza na Wanahabari (Hawapo pichani wakati wa utambulisho wa onesho hilo la msimu wa sita la SiTE linalotarajiwa kuanza Oktoba 21, Mlimani city Jijini Dar es Salaam.

Alisema Bw. Felix John.   SiTE 2022 litahudhuriwa na waoneshaji zaidi ya 200 na wanunuzi wa Kimataifa takribani 100 kutoka masoko ya kimkakati hususani nchi za Marekani, Uholanzi, Afrika Kusini,India, Urusi, Hispania, UAE, Poland, Finland, Japan, Oman na zingine nyingi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James ambaye kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  aliwahakikishiwa watu wote kuwa wamejiandaa kwa tamasha hilo ikiwemo kuimarisha hali ya ulinzi na usalama huku akiwakaribisha watu wote kutembelea maonesho hayo  kwa gharama nafuu kabisa ambapo watajifunza, watanunua bidhaa na pia watapata burudani mbalimbali. 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Bw. Felix John (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James wakati wakipitia mabanda ndani ya Mlimani City Jijini Dar es Salaam yatakapofanyika maonesho ya Utalii ya SiTE2022

Onesho hilo ambapo kiingilio kinatarajiwa kuwa Tsh . 5,000 kwa watoto na Wakubwa Tsh. 10,000 huku pia kutakuwa na kifurushi cha familia ambacho kitajumlisha Baba, Mama na watoto wawili ambapo ni Tsh 25,000.   Wadau waliodhamini onesho hilo ni pamoja na Wadau mbalimbali katika sekta ya Utalii, ikiwemo Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA), ambaye ni mdhamini mkuu wa juma Vodacom Tanzania, , Kampuni ya ONA& METAS Stories, CRDB, TATO, na wengine wengi.

Hata hivyo, onesho hilo ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo program maalum ya Tanzania-The Royal Tour iliyohasisiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kutangza vivutio vya Utalii na fursa zilizopo nchini za uwekezaji.   Mwisho.

Post a Comment

0 Comments