HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI HUU MWINGINE

 




Na Mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:


1) Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

2) Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

3) Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments