HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKENDA AAGIZA WALIMU SHULE YA MODERN ISLAMIC WATIMULIWE

 




Na Amedeus Somi

DAR ES SALAAM


Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia Mhe.Adolph Mkenda mapema leo hii ameagiza walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya Modern Islamic ya Pwani kutimuliwa kazi kwa kuonyesha udanganyifu katika Mtihani wa Darasa la Saba iliyofanyika mwezi Septemba.


Hiyo imekuja kufuatia taarifa zilizosambaa za Mwanafunzi Itsam Suleiman aliyebadilishiwa namba yake ya Mtihani.


Akizungumza na waandishi wa Habari Mhe. Waziri amesema Baada ya Timu ya Uchunguzi iliyoundwa ikisaidiana na Jeshi la Polisi wamebaini uzembe kwa watumishi na wasimamizi wa Mitihani hiyo hivyo kama  Wasimamizi wa Elimu wametoa Agizo la kufukuzwa kazi kwa Watumishi wote waliohusika pamoja na Walimu wa Shule hiyo.


“Chalinze Modern Islamic inafungiwa kuwa kituo cha mtihani kwa sasa


Kwa wale watumishi wa serikali tumewaandikia barua na nina imani watafukuzwa kazi


Mwenye shule na Waalimu wa Shule hiyo wafukuzwe kazi na kama wasipofukuzwa tutawasiliana na Kamishna wa Elimu wote wafukuzwe kazi


Pili waalimu hawa walikuwa wanafanya kazi shule binafsi wafukuzwe kazi la sivyo tunafutia usajili Shule hii”


Kilichofanywa na Wizara


Wizara Ilianza kwa mambo yafuatayo


Walianza na Mwanafunzi aliyebadilishiwa namba ya mtihani


Hatua

Kuwasiliana na kamati kufanya uchunguzi

Kuangalia script ya wataalm toka Jeshi la Polisi

Mtuhumiwa alifanya mitihani 5 kwa kutumia namba 40 somo la mwisho alitumia namba39.

Uchunguzi ulibaini watahiniwa 4 Walibadilishiwa. No


Justine abdallah 41

Kutumia namba 40


Jacob nassoro 40-41

Lailat 30-44


Mruma na 39-40


Dosari


Uzembe wa watumishi wafuatao


Mudy Elfance Mndelwa-Msimamizi Mkuu

Vitalis Kindole-Msimamizi

Amran Bakari Ramadhan (Mwl Mkuu)


Uchunguzi 


Mwandiko wa mtaniniwa 33 umefanana na mtahiniwa namba 34


Mwandiko no 34 unafanana na mwandiko wa aliyetumia no 33


Mwandiko wa mtahiniwa no 39 unafanana na aliyefanya mtihani aliyefanya kwa no 43



Jumla ya watahiniwa 7 walibadilishiwa namba za Mitihani


Matokeo


Baraza limefanya marekebisho ya namba za kila mtahiniwa ili aweze kupata matokeo halali.


Limefanya marekebisho hayo kulingana na uchunguzi wa Jeshi la Polisi.



Mitihani


Mitihani ya Taifa ya Darasa la nne inatarajiwa kuanza

26 na 27 Oct


Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili

Jumla ya Shule 5288.


TAZAMA VIDEO HAPA CHINI




Post a Comment

0 Comments