HEADLINES

6/recent/ticker-posts

YANGA YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA UNICEF

 

Na Amedeus Somi

Dar Es Salaam

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam leo hii imeingia mkataba wa miezi sita na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto - UNICEF unaolenga kuongeza uelewa kwa Umma kuhusu Chanjo ya UVIKO-19 na uhamasishaji kuhusu virusi vya EBOLA. 

Akizungumza katika makabidhiano hayo Rais wa Klabu hiyo Mhandisi Hersi Said Amesema

“Ni matunda kati ya Yanga na kampuni ya Jackson Group, Siku zilizopita Yanga walisaini mkataba wa masoko na Jackson Group.

Aidha amesema klabu ya Yanga imetengeneza mfumo mzuri wa kusaidia jamii ndio maana Unicef wakashawishika kufanya nao kazi

Ni mkataba ambao utaunganisha jamii na Unicef

1. Vita dhidi ya Covid 19

2.Yanga itafanya kazi na Unicef katika kutoa elimu juu ya janga la Ebola.

Mshirika huyo ambaye ni Unicef ameona watu wenye jukumu la kufanya kazi hii ni Yanga Afrika.

Aidha klabu ya Yanga imefanyiwa ukaguzi wa mashirikia mbal mbal iliwemo PWC yote hii ni katika kupata hati safi”

Makabidhiano ya mikataba hiyo imefanyika katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments