HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MADIWANI UBUNGO WAOMBA KIKAO CHA BARAZA KIAHIRISHWE



Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM

Baraza la madiwani Katika Manispaa ya Ubungo wameomba baraza liahirishwe wakakae kama kamati ili kujadili miradi ambayo haitekelezeki

Akizungumza baada ya kuahirishwa kikao cha Baraza hilo Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Ccm Wilaya ya Ubungo amesema kubwa zaidi iliyopelekea wao kuomba kuahirishwa ni kwa baadhi ya miradi kucheleweshwa na mingime kutofanyiwa utekelezaji.


                                                   Edward Laizer Diwani Kata ya Saranga


Edward Laizer Diwani Kata ya Saranga amesema  wakiwa wamebakisha mwaka mmoja tangu wamepewa dhamana ya kunadi ilani ya Chama cha Mapinduzi hamna kitu watakachowaeleza wananchi katika Kata zao. Aidha ameendelea kusema kuwa Hata Greda la kuchimba barabara limekuwa bovu hamna anayeshughulikia jambo hilo, Ameshangaa Halmashauri ya Ubungo inayokusanya Billioni 32 kushindwa kununua tairi mpya kwenye Greda.

Alex Masatu Kaimu Mhandisi Manispaa ya Ubungo amezungumzia kuhusu hali ya Greda lililoharibika alisema kuwa.

Greda hilo lilifanya kazi  tarehe 17 /11/2022 Kata ya Kibamba kwa muda wa siku mbili lakini baada ya hapo liliharibika na kurudishwa Manispaa kwa ajili ya ununuzi wa Matairi wakati huu wapo katika kutafuta mzabuni atakayeleta matairi hayo.

                          Alex Masatu Kaimu Mhandisi Manispaa ya Ubungo 


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Grace  Mwaigaga ambaye pia ni Mchumi wa Manispaa ya Ubungo amesema sio kweli miradi haitekelezeki  ni kwamba kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wanatekeleza kwa Bajeti.

Mpaka sasa Halmashauri imetoa Bil 2.7 kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.


                                 Mchumi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Grace  Mwaigaga


Bofya link hapa kutazama Video



Mwisho. 



Post a Comment

0 Comments