HEADLINES

6/recent/ticker-posts

DITOPILE AMPONGEZA RAIS SAMIA UJENZI MABWENI YA WENYE MAHITAJI MAALUM


Na Mwandishi Wetu,

DODOMA,

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza Sh Bilioni 960 zilizokua zimetengwa kwenye bajeti ya sherehe za uhuru ili zikatekeleze ujenzi wa mabweni ya Shule za Wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Ditopile ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , George Simbachawene iliyoeleza maelekezo hayo ya Rais Samia.

Ditopile amesema uamuzi huo wa Rais Dk Samia umeonesha ni jinsi gani ambavyo ana mapenzi makubwa na watanzania hasa katika sekta ya elimu kwa kufuta sherehe za uhuru mwaka huu na fedha zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho hayo kuelekeza ziende kwenye sekta ya elimu na hasa kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum.

" Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo anayo nia ya dhati ya kuwajali, kuwapenda na kuwajengea mazingira safi na rafiki wanafunzi wenye mahitaji Maalumu kwa uamuzi wake wa kishujaa kafanya Leo.

Kwa Niaba ya Wanawake wa Mkoa wa Dodoma Nampongeza sana Rais Samia Kuelekeza Bilioni 960 ambazo zilitengwa kwenye Bajeti kwa ajili ya Sherehe za Uhuru Mwaka Huu kwenda kujenga Mabweni Shule za wanafunzi wenye mahitaji Maalumu," Amesema Ditopile.

Ditopile amesema kwa muda mrefu Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma Shule zisizo na mabweni wamekua wakipata changamoto ya namna ya kufika Shuleni lakini uamuzi huu wa Rais Dkt Samia kuwajengea mabweni utarahisishia upatikanaji wao wa elimu na umeonesha utu na upendo ndani yake.

" Kwa Niaba ya Wanawake wa Mkoa wa Dodoma Nampongeza sana Rais Samia Kuelekeza Bilioni 960 ambazo zilitengwa kwenye Bajeti kwa ajili ya Sherehe za Uhuru Mwaka Huu kwenda kujenga Mabweni Shule za wanafunzi wenye mahitaji Maalumu," Amesema Mbunge Ditopile.

Post a Comment

0 Comments