HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RC TABORA AFUNGUA MAJADILIANO BIASHARA YA ASALI


 Na Mwandishi Wetu

Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kwa kushirikiana na wataalam wa nyuki na maafisa ushirika pamoja na wadau wengine wamejadili mfumo wa stakabadhi za ghala kwa maendeleo ya biashara ya asali wilayani Sikonge na Tabora kwa ujumla.

Katika majadiliano hayo Dkt. Batilda aliweza kufahamu kwa kina juu ya mfumo huo ambao kwa hakika unakwenda kupunguza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa mazao ya nyuki. Na kwamba mfumo huo utakwenda kufanya kazi chini ya usimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge kwa kushirikiana na wadau wengine.

Aidha Dkt.Batilda alifanikiwa kufahamishwa na walaam faida za mfumo huo ambao utakwenda kumkomboa mfanyabiashara wa mazao ya nyuki kwa Kuchochea ongezeko la uhitaji na bei ya asali, kukuza pato la Serikali kutokana na kodi zitakazopatika kutokea kwenye uongezaji thamani na ukuaji wa pato la mtu mmoja mmoja, kukuza pato la halmashauri kutokana na faida itakayopatikana kwenye kampuni, ada itakayopatikana kwenye uchakataji, ushuru wa bidhaa na faida nyingine za kiuchumi zinazotokana na uchakataji.

Na zaidi ni kwamba mfumo huo utapanua wigo wa ajira kupitia viwanda vidogo vya uchakataji hususanimaeneo ya vijijini kama vile wasimamizi wa kiwanda, wabeba mizigo, warina asali, watengeneza mizinga na wengineo, kukuza biashara kama vile usafirishaji, ufundi mitambo, chakula na huduma nyingine zinazosaidia viwanda vidogo vidogo kufanya kazi, Kuchochea ukuaji miji kutokana na shughuli za uchakataji utaoleta wageni na wapitaji kwenye eneo ambalo linafanya shughuli za uchakataji.

Ili kuhakikisha mfumo huu unafanya kazi ipasavyo, Dkt.Batilda amewataka watendaji ngazi ya mkoa na wilaya kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi ambayo yatasaidia mfumo huu kufanya kazi. Na kama kiongozi wa mkoa atahakikisha mazao ya nyuki yanakuwa na tija kupitia mfumo huu wa stakabadhi za ghala.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments