HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MADUME YA NGOMBE 50 AINA YA BORANI YAGAWIWA KWA WAFUGAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA





Na Mwandishi Wetu,

MKURANGA,

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir Ally Leo 28.03.2023 amekabidhi Madume Bora ya N'gombe 50 aina ya Borani kwa wawakilishi wa Vikundi vya Wafungaji waliopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.   Lengo kuu la ugawaji wa Madume hayo ni kwa ajili ya kuimarisha ufugaji bora wenye tija na kibiashara. 

Hafla hiyo imefanyika katika Kijiji cha Mkwalia na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mwantum Mgonja, Watalaamu wa Sekta ya Mifugo, Wafugaji na Wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga.

Post a Comment

0 Comments