HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MASHINDANO MAKUBWA YA QURAN KUFANYIKA UHURU APRILI

 Na Amedeus Somi,

DAR ES SALAAM,

Mapema leo hii Viongozi wa Dini ya Kiislam wamezungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya mashindano makubwa ya kuhifadhi Quran Tukufu yanayotarajiwa kufanyika Aprili hii katika Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari Mwenyekiti wa Taasisi ya Ayshah Sururu Foundation Bi.Aisha Sururu amesema  mashindano hayo ya Kitaifa ya Quran yanatarajiwa kufanyika Aprili 2 Katika Uwanja wa Uhuru huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekitiwa Taasisi ya Ayshah Sururu Foundation Bi.Aisha Sururu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya kuhifadhi Quran Tukufu Tanzania Sheikh Nurdeen Kishki Amesema anashukuru Wizara kwa kutoa Ushirikiano mkubwa kwani wameruhusiwa kutumia Uwanja wa Uhuru ambapo watamwaga maturubai Kwenye eneo la Kati kati ya Uwanja (Pitch).Aidha Sheikh Kishki amesema Mashindano makubwa ya Quran kwa ngasi ya Afrika yanatarajiwa kufanyika Aprili 9 katika Uwanja wa Uhuru kaulimbiu ya Mashindano hayo ni ALLAH ANA WATU NA WATU WAKE NI WATU WA QURAN

Mgeni rasmi katika Mashindano hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Aidha Sheikh Kishki amesema mashindano makubwa ya Kimataifa ya Quran ya Dunia yanatarajiwa kufanyika Aprili 16 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Uwakilishi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Naye Mstahiki Meya Wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omary Kumbilamoto amewaomba Waislam na Wtanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo.


Post a Comment

0 Comments