HEADLINES

6/recent/ticker-posts


Na Mwandishi Wetu
TABORA

Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Balozi Batilda Salha Burian amewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kuchangamkia fursa za matibabu zinazotolewa na hospitali zetu zilizopo mkoani Tabora.

Ameyasema hayo alipotembelea hospitali ya rufaa ya Nkinga iliyopo wilayani Igunga, mkoani Tabora, ambapo pia alipata wasaa wa kuwajulia hali baadhi ya wagonjwa. 

Sambamba na hilo ametoa pongezi kwa uongozi mzima wa hospitali ya Nkinga kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa huduma za afya zenye ubora, hususani matibabu ya Fistura ambayo hutolewa bure, na pia wagonjwa hupatiwa nauli ya kufika hospitalini na nauli ya kurudi nyumbani baada ya matatibabu kukamilika.


Sambamba na hilo ametoa pongezi kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya Nkinga pamoja na wadau wa sekta ya afya mkoani Tabora kwa kuleta madaktari bingwa ambao kwa hakika wamekuwa msaada.

Post a Comment

0 Comments