HEADLINES

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA MILLIONI 900 ZATOLEWA KWA WAJASIRIAMALI KIGAMBONI

 Na Amedeus Somi,

KIGAMBONI DAR ES SALAAM,


Zaidi ya Millioni 900 zimetolewa kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo kwa wajasiriamali Katibu Tawala wa Manispaa ya Kigamboni Bi. Pendo Mahalu  ambaye amemumwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Zainab Abdallah Bulembo amewapongeza wafanyabiashara wa Kigamboni kwa kufikia hatua hiyo kubwa ya kimaendeleo.

Amesema ni matumaini yake kuwa fedha hizi zitakwenda kutatua changamoto ya mitaji kwa wajasiriamali hao kwani ni fedha ambazo zinatolewa kwa masharti laini bila riba yoyote.

Nyinginezo

SAUDI ARABIA KUWEKEZA SEKTA YA MIFUGO NCHINI

Aidha amesema changamoto kubwa ni urejeshaji wa fedha hizi za mikopo akiwataka wanufaika wa mikopo hiyo kuondoa dhana ya kuwa fedha za mikopo ni za serikali ni kama za sadaka tu. amewataka kutumia fedha hizo kwa kufanyia matumizi waliyokusudia na sio vinginevyo.

Bi Veronica Kiluvia ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Be.Erasto Kiwale amesema nia ya serikali ni kuwanufaisha na kuwawezesha wananchi kupitia vikundi hivyo kwa kupitia vikundi serikali itawezanluwafikia wajasiriamali wengi.

Asha Nassor afisa Ukaguzi kutoka mfuko wa mfuko wa taifa wa jamii NSSF Amesema  wajasiriamali wana uwezo wa kuweka akiba  kwenye mfuko wa jamii ambapo kima cha chini kikiwa ni shilingi elfu ishirini kwa mwezi ambayo haitakuwa na makato.

Kwa upande wa wanufaika wa mikopo hiyo wamesema wanaishukuru serikali ya awu ya sita kwa kuwapa mikopo hii ya asilimia kumi ya  mapato ya ndani.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments