HEADLINES

6/recent/ticker-posts

STAMICO WAJIPANGA KUWAFIKIA WACHIMBAJI WADOGO NCHI NZIMA

 


Na Mwandishi Wetu,

DAR ES SALAAM

*Dkt. Mwasse awataka Wadau kusukuma Ajenda ya Viwanda kupitia Sekta ya Madini*

*DACOREMA Watoa Wito Wadau Madini ya Viwandani kushiriki mkutano kujadili changamoto*

*CTI Yasisitiza Viwanda kutumia Malighafi za Ndani*

*TAWOMA Yasifu Mabadiliko ya STAMICO kama Mlezi wa Wachimbaji Wadogo*

Katika kuhakikisha Tanzania inanufaika na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Duniani kupitia Sekta ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeazimia kuwafikia Wachimbaji Wadogo wa Madini nchi nzima ili kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo masoko, kupatiwa elimu kwa lengo la kuongeza kiwango cha uzalishaji wa madini wanayoyazalisha.

Hayo yamebainishwa Aprili 4, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar esSalaam ikiwa ni maandalizi ya kufanyika kwa mkutano wa Wachimbaji Wadogo na Wadau wa Madini ya Viwandani Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani utakaofanyika tarahe 5 na 6 jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko.

Akifafanua kuhusu mkutano huo, Dkt. Mwasse amesema, umeandaliwa na STAMICO kwa kushirikiana na Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (DACOREMA) pamoja na Shirikisho la wenye viwanda ambapo pamoja na mambo mengine unalenga kujadili na kuweka mapendekezo ya utatuzi wa changamoto zinazokabili uchimbaji na biashara ya madini ya viwandani hususan masoko, mitaji na zana za uchimbaji.

‘Tumenunua mashine za uchorongaji kupata sampuli. Sekta za uzalishaji zimepewa kipaumblele na sisi tunataka Sekta ndogo ya uchimbaji iunge mkono na inufaike zaidi,’’ amesisitiza Dkr. Mwasse.

Ameongeza kwamba, mkutano huo unatarajia kuwakutanisha wachimbaji wadogo, wamiliki wa viwanda ambao ni watumiaji wa madini ya viwandani, taasisi za fedha, wasambazaji vifaa na wasimamizi sheria, wasimamizi wa kodi na hivyo kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau wa madini kujitokeza kushiriki mkutano huo ili kuwezesha kusukuma mbele ajenda ya viwanda kupitia Sekta ya Madini

Post a Comment

0 Comments