HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA AL-HIKMA YATOA VIGEZO KWA WATAKAOLIPIWA MAHARI


Na Amedeus Somi,

DAR ES SALAAM,

TAASISI ya Al-Hikma, ambayo ndio waandaaji wa Mashindano ya Kuhifadhi Quraan Afrika,imewataka vijana wenye nia ya dhati ya kufunga ndoa kujitokeza kuchukua fomu ili kulipiwa mahari na taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam,, Mkurugenzi wa taasisi hiyo  Sheikh Nurdeen Kishk ametolea ufafanuzi wa suala la kulipia mahari la kuwalipia mahari vijana 50 wenye nia ya kuoa lakini ambao hawana uwezo wa kulipa mahari kama alivyotangaza siku chache zilizopita

 Sheikh Kishk amesema kuwa utaratibu huo utafanikishwa kwa vigezo maalumu ambapo alitaja vigezo nane.

Sheikh amesema lazima wawe waumini wa Dini ya Kiislamu,awe raia wa Tanzania, awe amelipa posa,asiwe ameoa,awe amejaza fomu maalumu inayotolewa na Al Hikma na awe amefanyiwa usahili katika taasisi  hiyo.

Alisema, ndoa zote 50 zitafungiwa jijini Dar es Salaam na Mufti Sheikh Mkuu wa Tanzania Dk.Abubakar Zubeiry.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma Sheikh Nurdeen Kishki akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dae es Salaam.(PICHA NA AMEDEUS SOMI)

Hata hivyo Sheikh Kishki ameongeza kuwa kigezo kingine ni lazima mwisho ashawishi ndugu na baba wa mwanamke anayetaka kumwoa ahudhurie ndoa hiyo jijini Dar es Salaam,"

Alieleza, baba wa mwanamke kuhudhuria ufungaji ndoa ni muhimu akiwa kama walii ingawa binti anayeolewa siyo lazima kuhudhuria kwa mjibu wa mwongozo wa dini ya kiislam.

Hata hivyo Sheikh Kishk amesisitiza kuwa ni muhimu wanaohitaji kupewa mahari na Al Hikma kuwa na nia ya dhati ya kuoa.

Amefafanua , tangu Aprili 9 mwaka huu alipotangaza dhamira ya taasisi hiyo kuwalipia mahari watu 50 zaidi ya maombi 1000 kutoka ndani na nje ya nchi yamepokelewa yakiwemo ya wanawake watatu.

Ameeleza tayari Taasisi imeanza kutoa fomu maalumu zenye vigezo,vambazo zinatolewa  katika ofisi zote za Al Hikma yenye makao yake makuu Mtaa wa Yombo wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

Fomu zitatolewa Dar es Salaam, hivyo wanaoomba watatakiwa kufika wao wenyewe au ndugu zao kuchukua fomu.Ni muhimu wao kufika ili tuwape,tuwatathimini na kuwahoji.

Sheikh Kishk alisema, Al Hikma itagharamia mahari, mavazi kuandaa sherehe ya harusi,chakula na vinywaji.

Kishki amesema kuwa Taasisi hiyo itatoa mwaliko wa watu 10 kutoka upande wa mwanaume na watu 10 upande wa mwanamke .

Amesema wamechukua hatua ya kujitokeza kulipa mahari kwa watu 50 ikiwa ni shukurani zao baada ya Mashindano ya Kuhifadhi Quraan Afrika na kuwaepusha vijana dhidi ya mmomonyoko wa maadili. 


Tazama Video Hapa

https://youtu.be/cQNcHWmK5Eo


Post a Comment

0 Comments