HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MASANJA ACHANGISHA MILIONI 95 ZA UJENZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO SDA PASIANSI MWANZA

 


Na MwandishI Wetu,

MWANZA,

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja  ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya ibada ya Kanisa la Waadventista Wasabato SDA Pasiansi kwenye Jimbo Kuu la Nyanza Kusini mkoani Mwanza na kupata kiasi cha shilingi milioni 95. 2 ambapo  fedha taslimu zilikuwa shilingi milioni 47.3 na ahadi shilingi milioni 47.8.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Masanja amelipongeza kanisa la SDA Pasiansi kwa kuanza ujenzi wa kanisa hilo jipya ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2022 huku waumini wa kanisa hilo wakiwa wameshafanikiwa kuchangia shilingi milioni 56 za ujenzi.

"Serikali inatambua mchango wa kanisa hili katika sekta ya Elimu na Afya. Ujenzi wa kanisa hili ni wito na wajibu wa kila mmoja wetu"  amesema Mhe. Masanja

Amesema lengo kuu la kufanya harambee hiyo ni kutafuta fedha za ujenzi wa kanisa na fedha zinazohitajika ni zaidi ya milioni 200. 

 Amewaomba waumini wa kanisa hilo waendelee kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo na pia kuendelea kuiombea Tanzania iendelee kuwa na  amani, umoja na upendo.

Naye, Mchungaji wa Kanisa la SDA Pasiansi Harun Kuyenga amesema mradi huo wa ujenzi la kanisa ulianza mwaka 2022 na unatarajia kukamilika mwaka 2024 na mara baada ya kukamilika kwake kanisa  litakuwa na uwezo wa kubeba waumini 3000 ambapo  kanisa la sasa lina uwezo wa kubeba waumini 800.

 Ameongeza kuwa  wameamua kujenga kanisa hilo jipya  kutokana na ongezeko la waumini kutoka maeneo tofauti tofauti huku akisisitiza kuwa kwa sasa kiasi cha fedha shilingi milioni 200 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo.

Katika Harambee hiyo, Mhe.Masanja pamoja na familia yake na marafiki zake walifanikiwa kuchangia ujenzi wa kanisa hilo kiasi cha shilingi milioni 51,050,000 ambapo fedha taslimu ilikuwa ni shilingi milioni 30,550,000 na ahadi shilingi milioni 20,500,000.




Post a Comment

0 Comments