HEADLINES

6/recent/ticker-posts

BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA YATOA MAFUNZO UTEKELEZAJI MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA .

 


Na Mwandishi Wetu,

DAR ES SALAAM

 Mafunzo hayo yanayofanyika kila mwaka  nchini yenye  lengo la kuwajenga uwezo  Watendaji  wa Kampuni za waendesha ghala,  Wasimamizi wa Ghala,  Meneja Dhamana  pamoja na washiriki binafsi yamefunguliwa na Mkuu wa  wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba leo Tarehe 28 Agosti 2023, katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa  Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mhe.  Komba alieleza kuwa  Mafunzo haya yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa  Wadau wote, vilevile ameitaka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Pia , mafunzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu pamoja  na  Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji  wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Mary Fidelis.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa  Stakabadhi  za Ghala  Bw. Asangye N. Bangu amesema kuwa  lengo kubwa ni kuongeza tija katika ufanyaji   kazi na matarajio ya mafunzo  hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa  kwa usahihi kwa kuzingatia sheria .

Aidha Mhe. Bangu  ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo watatekeleza shughuli zao za kiserikali pia wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya  hivyo, Washiriki  waliojitokeza kupata mafunzo haya  watapatiwa cheti cha kufudhu usimamizi wa shughuli za uendeshaji Ghala  ambacho  kitatambuliwa na  Bodi ya Stakabadhi za Ghala.

Post a Comment

0 Comments