HEADLINES

6/recent/ticker-posts

HUDUMA ZA MAWASILIANO KUNDUCHI-MTONGANI ZAREJEA

Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM,

Mawasiliano ya barabara ya Kunduchi Mtongani yamerejea kufuatia kukatika kwa kingo ya daraja la mto Tegeta kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maendeo mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua kazi ya kurejesha huduma kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika na mvua jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Ujenzi  Mhandishi Godfrey Kasekenya amesema serikali imejipanga kukabiliana na changamoto zinazojitokeza na kutoa wito kwa wakala wa barabara nchini Tanroads kuendelea kufanya kazi kwa haraka ili kurudisha huduma kwa wananchi.

"Nitoe tahadhari kwa Tanroads Mkoa kukagua hasa maeneo ya madaraja mnapoona kuna changamoto yoyote inayotokea ili kuokoa maisha ya vyombo na watu muwe haraka kutoa tahadhari kwa sababu nyie ndio mnajua hivyo tusione shida kuweka alama za tahadhari hakikisheni mnapita kila maeneo"

Aidha katika hatua nyingine Mhandisi Kasekenya ametoa wito kwa wananchi kuacha kujenga pembezoni mwa kingo za mito kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kongezeka kwa njia za maji.  


Mkuu wa kitengo cha Matengenezo wa  Tanroads  Mkoa wa Dar es Salaamk Mhandisi Suzana Lucas

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Matengenezo wa  Tanroads  Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Suzana Lucas amesema kazi kubwa iliyofanyika ni kujaza mawe na kuelekeza maji kurudi katika mkondo wake kwani wingi wa maji yaliyoambatana na magogo ndio kilichopelekea kukatika kwa tuta linalounganisha barabara na daraja.

Daraja la Kunduchi Mtongani ambalo lilipata madhara 

Ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Ujenzi imepita kukagua miundominu katika maeneo ya Jangwani, Kinondoni Mkwajuni, Kunduchi Mtongani  Mbweni na  Mpiji.


Post a Comment

0 Comments