HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU MAGONJWA YALIYOKUA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendesha kikao kazi kwa  waandishi wa habari ili  kuwa na uelewa juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Kikao kazi hicho ambacho kimeendeshwa na Mpango wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kimefanyika katika ukumbi wa  Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Akizungumza katika kikao kazi hicho Afisa mradi wa mpango huo kutoka Wizara ya Afya Dkt. Isaack Njau amesema kama  Magonjwa haya ni Matende na Mabusha, Kichocho , Minyoo ya Tumbo n kibofu cha mkojo, Usubi na Trakoma.

‘’Kama Wizara tumekuwa tukipambana nayo takribani miaka 20 iliyopita na tumeona ufanisi mkubwa kwenye ugonjwa wa matende na mabusha maambukizi yamepungua kwenye Wilaya 112 ambapo hatumezeshi tena kinga tiba tumebakiwa na Wilaya 7 tu na Trakoma tumebaki na Halmashauri 9’’

 Aidha Dkt. Njau ameendelea kusema kuwa katika ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo wameweza kupunguza maambukizi kwenye baadhi ya Kata na sasa wanatoa dawa pale ambapo maambukizi yanaonekana kuzidi.

Magonjwa haya yanapatikana kwa kiwango kikubwa katika baadji ya maeneo mfano ugonjwa wa kichocho upo zaidi katika mikoa ya kanda ya Ziwa na Ugonjwa wa Matende unapatikana zaidi katika mikoa ya Pwani, kama Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Lindi.

Kwa upande wake Mratibu wa magonjwa hayo kutoka Wizara ya afya Dkt. Clara Mwansasu amesema kabla ya kuanza utekelezaji wa afua za magonjwa hayo kama Wizara walifanya tathmini na kugundua magonjwa haya yameenea katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na viashiria vyake.

‘’Matende na mabusha katika tathmini ya awali ulionekana umeenea katika halmashauri 119 hadi kufikia mwaka 2003 ni halmashauri 7 tu zimeendelea kuwa na ugonjwa huo na ugonjwa wa usubi umeonekana kushamiri katika Halmashauri 28 zenye ukanda wa  mabonde na milima yenye vyanzo vya maji licha ya kuwa mpaka sasa maambukizi yameshuka kwa kiasi kikubwa’’

Dkt.Clara ameongeza kuwa katika ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo wameweza kushusha ukubwa wa tatizo ambapo kwa tathimi ya awali ulinea katika Halmashauri 184 japo bado wanaendelea kufanya afua katika halmashauri zote ili kushusha ukubwa wa tatizo.

Malengo ya kikao kazi hicho ni kujenga uelewa kujua afua mbalimbali katika kutokomeza magonjwa hayo, waandishi wa habari kuwa  na uelewa sahihi wa kiutoa taarifa za maonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

 Kaulimbiu ya Mpango huo ni Tuungane tuchukue hatua tutokomeze magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele.

Maadhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele  yatafikia kilele 30 Januari mwezi huu.

Kinachofanywa na Wizara kwa sasa ni umezeshaji wa kingatiba kwa walengwa

Kuboresha usafi wa mazingira

Huduma za matibabu kwa walioathirika.

Kupambana na wadudu waenezao magonjwa ya kuambukiza

Kutoa elimu kuhusu kushiriki na kupambana na magonjwa haya.

Post a Comment

0 Comments