HEADLINES

6/recent/ticker-posts

ERB YAOMBA SERIKALI BILLIONI 16.5 KUJENGA SHULE YA WAHANDISI


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imeiomba serikali fedha kiasi cha zaidi ya Billioni 16 ili kusaidia katika mchakato wa kuanzisha shule ya wahandisi (School of Professional Engineers).

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika programu ya mafunzo kwa vitendo kwa wahandisi wahitimu yaani SEAP (Structured Engineers Apprenticeship Programme )iliyofanyika kuanzia tarehe 26 na kumalizika leo Februari, 28 2024 msajili wa Bodi ya Wahandisi  Mhandisi Bernard Kavishe  amesema bodi ipo katika mkakati wa kuanzisha shule hiyo hivyo wanaomba serikali kuishika mkono.

“Mkinipa Billioni tatu nawajengea School of Engineering ni shule ya Uwinguni, Shule ya mtandaoni lakini itaenda zaidi site, kwa wale vijana ambao wapo kwenye mafunzo ambao hawana ufadhili wanahitaji Billioni tatu kila mwezi na walioko nyumbani wangepata ufadhili”

“Billioni 10 tutakapoanza kuwasaidia hawa walioko kwenye mafunzo  na wengine wengi bado wapo nyumbani hawajajitokeza kwa mwaka wanamaliza wahandisi 3500 wa ndani na nje, hiyo kama ni mpango wa miaka mitatu tunaongelea wahandishi 10,500 wale kuwatunza kwa mwezi mmoja ni Billioni 10 hivyo Billioni 120 kwa mwaka, hivyo mpango huu tungefanya asilimia mia moja ya usaidizi na ingetupeleka mbali sana na ingerudi kwa sababu wangetumika kwa jamii”

 

Kavishe ameongeza kuwa kwa mwaka huu wanategemea kupeleka masomoni wahandisi 1200 licha ya kuwa watakaomaliza ni 3500 na kwa leo tayari wameshapatikana 400.

Mhandisi Kavishe ameongeza kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa wahandisi kama 12,000 kwani kama nchi tunavyozidi kukua na ndio mahitaji yanaongezeka.

“Mpango wa kuandaa wahandisi tunao na tunauita “Kupanda Mbegu Mapema” mbegu ya uandisi inapadwa mapema tangu kidato cha pili kwa sababu pale ndio wanafunzi wanajigawa tunawaambia wanaopenda kuwa waandisi ni lazima wasome Sayansi hivyo tunawahamaisha wachukue masomo hayo”

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania Mhandisi Gemma Modu amewaasa wahitimu kutumia ujuzi na elimu waliyopatiwa kutumika kwa tija kwa ajamii na Taifa kwa ujumla.

“Hivyo basi nawaasa mzingatie yote mliyofundishwa katika semina hii elekezi na kila somo lililojumuishwa linachangia katika kujenga msingi imara wa safari ya kuelekea kuwa Wataalamu na katika kazi zenu za baadae, kuwa na ufahamu wa hisia, kudumisha tabia njema na mtazamo chanya Pamoja na kufata maadili ya kitaalamu ni mambo muhimu kwa mafaniko yetu na hasa katika hii safari ambayo tunaelekea kwenda kuwa wataalamu kamili”.

Wadau wa Semina hiyo kutoka Bara na Visiwani wameshukuru waandaaji wa semina hiyo ambapo wamesema itawasaidia sio tu kwao bali Taifa zima katika kusonga mbele kiuchumi.


Shule hii ni muendelezo wa mradi wa SEAP ambayo italenga wahandisi kuweza kufikia vigezo vya kusajiliwa katika nyanja ya Mhandisi mwelekezi, msimamizi wa miradi, Mhandisi mahiri na utambuzi wa ujuzi kwa mafundi.


Baadhi ya wahandisi wahitimu wakifatilia kwa karibu mafunzo katika ya programu ya mafunzo kwa vitendo kwa wahandisi wahitimu yaani SEAP (Structured Engineers Apprenticeship Programme ) (Picha na Amedeus Somi)




Post a Comment

0 Comments