HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATOA MAJIBU SANAMU YA MWALIMU NYERERE KUTOFANANA NAYE

 


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Balozi Shaibu Said Musa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema sanamu ya Hayati Mwalimu Nyerere imefanana kwa asilimia 92 na uhalisia wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024 amesema Serikali imefata maelezo ya kitaalamu iliyotolewa na Kamati Maalum ambayo ilishiriki tangu mijadala mpaka kupatikana kwa ile sanamu ambayo imefadhiliwa na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika SADEC kwa wazo ambalo lilitolewa na Viongozi mbalimbali wa Afrika ikiwemo Hayati Robert Mugabe enzi za uhai wake.

Taswira ya Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyowekwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa kwa ajili ya kutambua mchango wake katika masuala ya ukombozi Barani Afrika 

“Kuhusiana na sanamu kweli kumekua na mixfillings na reactions ambazo wapo wanasema kwamba kuna hitilafu lakini nataka mjue tu kwamba upande mmoja wana mawazo hayo lakini wapo wengine  upande wa pili wapo wenye kukubali na kusema kwamba ni Mwalimu Nyerere.

Aidha Balozi Said Mussa amesema Mtoto wa Hayati Nyerere Madaraka Nyerere naye alikuwepo katika uzinduzi ule ambapo alisema kuwa sanamu ile inafanana kabisa na baba yake na kama mtu anataka kujua Zaidi amtafute na kumuuliza.

“Mwalimu mnayemuona katika sanamu ile ya Addis ni wa miaka ya 60-80 akiwa yupo Active katika mapambano ya kusaidia kuleta uhuru na maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika”.

“Kauli ya mwanaye ameendelea kusisitiza kwamba yule ni baba yake na kama kuna mtu anataka amtafute amuulize”

Taratibu za kitaalamu zinasema kwamba inatakiwa uipatie angalau asilimia 75 ya sanamu unayoitengeneza katika utengenezaji wake na ile sanamu ya Addis (Mwalimu Nyerere) ni asilimia 92.



Post a Comment

0 Comments