HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TEKNOLOJIA KUTUMIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry William Silaa amesema serikali ipo katika mchakato wa mwisho ili kutumia mifumo ya Tehema katika kutatua changamoto za ardhi katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa yote nchini.

Waziri Silaa amesema mfumo huo wa Tehema unaandaliwa ili kurahisisha utendaji kazi katika kutatua changamoto za masuala ya ardhi Pamoja na usaidizi mbalimbali wa ardhi nchini.

“Tunayo timu kubwa ya wataalamu pale Arusha inayoanda mfumo ambayo Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametenga fedha na ametuwezesha na ametuelekeza kwahiyo upo mfumo wa Tehama unaandaliwa mfumo  ambao kesho hatutakuwa na marundo ya watu wanaokusanyika chini ya Maturubai wakifanya miamala ya ardhi, ukitaka kununua ardhi ukitaka kuomba hati utaingia kwenye simu janja yako utafanya miamala ya ardhi na itakamilika kwa muda mchahe na hatukakuwa na nafasi tena ya Waziri kuja kusolve tatizo ambalo linawez kutatuliwa na mfumo wa Tehema”

Katika hatua nyingine Waziri Silaa amewaasa wananchi kuwa na mazoea ya kuandika mirathi ili kuepuka madhila yatokanayo na ugawaji wa mali pindi mtu anapofariki.

“Nimeendelea kuziomba kuzisihi na kusisitiza familia zetu wale ambao wamejaliwa na Mwenyezi MUNGU Kuwa na Imani za Dini ambao wanaamini kuna kufa basi waandike wosia ili wapunguze usumbufu baada ya wao Kwenda mbela za haki, Binadamu yoyote anapofariki  ni lazima mirathi ifunguliwe mali zigawiwe na mirathi ifungwe tunaendelea kuwasisitiza Watanzania kuendelea kufungua mirathi ya watu waliotangulia mbele za haki”


Waziri huyo ameendela kusema na kuongeza kuwa yapo matatizo mengi ya ardhi hivyo kama Wizara itaendelea kuweka kambi mbalimbali na kwa kutumia mifumo ili kuondoa migogoro hiyo yenye sura nyingi.

Akitoa tathmini ya kliniki za ardhi za nchi nzima amesema tayari wamewaelekeza maafisa na makamishna wote wa  ardhi kwa ngazi za mikoa na wilaya watoke maofisini na Kwenda kutatua ero za ardhi kwa wananchi.

Kliniki hiyo ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mpaka sasa imeshafanya utatuzi, urasimishaji na utoaji wa hati katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma inatarajia  kumaliza Februari 25  katika Jiji la Dar es Salaam ambapo mpaka sasa tayari imeshatoa zaidi ya Hati elfu saba itaelekea katika Majiji ya Tanga, Mbeya, Arusha na Mwanza.

Joseph Edmund Mkazi wa Bunju ambaye amepatiwa Hati yake leo hii katika Kliniki hiyo


BOFYA HAPA KUONA VIDEO ðŸ‘‡ðŸ‘‡ðŸ‘‡

https://youtu.be/_2J0D8jXFIY


Post a Comment

0 Comments