HEADLINES

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI DAR LAMKAMATA SUKUNUNU01 ALIYESUMBUA X KUTUKANA VIONGOZI WAKUU


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata, linawashikilia na kuwahoji kwa kina watuhumiwa watano (5) kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali ya kimtandao.

Hii ni kutokana na ufuatiliaji maalum unaoendelea unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na makosa ya kimtandao. Waliokamatwa ni pamoja na Obadia Kwitega (35) mkazi wa Kigamboni na Issa Mwamba (28) mkazi wa Tabata Segerea.

Wamekamatwa kwa tuhuma za kumiliki televisheni ya mtandaoni ya kwenye Youtube iliyotambulika kwa jina la Jamii Digital, na akauti ya mtandao wa X iitwayo SUKUNUNU 01, waliyokuwa wanazitumia kusambaza taarifa za uongo na za uchochezi kuhusu viongozi wakuu wa Serikali. Baadhi ya taarifa zao zilisomeka “MKAKATI WA SIRI JANUARY MAKAMBA KUMNG’OA RAIS SAMIA 2025”

 Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limemkamata pia Frank Mbetu (35) mkazi wa Ligula, Mtwara kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Serikali ngazi ya Katibu Mkuu Kiongozi na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kuwa angewapa watu kazi serikalini au kupandishwa vyeo.

Amekamatwa pia Honest Mgona (47) mkazi wa Mabwepande kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kuwa ametumwa na Mhe. Mohamed Nchengerwa (MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa kusambaza mitungi gesi kwa wananchi na baadae kuwatapeli kwa kuwadai pesa za usafiri. Mwingine ni Edwin Kasebele@ Marlin (24) Mkazi wa Mapelele, Mbeya anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Ofisiya: - Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum, S.L.P.9140, DAR ES SALAAM …………… Simu: +255 (0) 22-2117705 Nukushi: +255(0) 22-2121 524 Baruapepe: utawala.dsmz@tpf.go.tz 23/01/2017 33 2 ‘Facebook’ na ‘Whatsapp’ kuwa anafanya biashara ya vitenge na hivyo kujipatia pesa kwa udanganyifu kutoka kwa watu mbalimbali.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na simu 7 na kadi za za simu 13 za makampuni mbalimbali ya simu ambazo wamekuwa wakitumia kama nyenzo kutekeleza uhalifu wao. Kutokana na vitendo hivi vya kihalifu kwa njia ya mtandao, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa rai kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao na Jeshi la Polisi linaendelea kuwachukulia hatua kali watu wengine wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za matumizi sahihi ya mitandao.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawahimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi kilicho karibu ili hatua stahiki zichukuliwe haraka. Jeshi la Polisi pia linawahimiza wananchi kuendelea kutotoa CV, namba ya NIDA au vitambulisho, nywila (password) au namba ya siri (PIN) kwa mtu yeyote bila kuwa na uhakika na kinachofanyika. Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la kuuwawa kwa mtoto wa miaka 7 mwanafunzi wa shule ya msingi Kibonde maji B, Mbagala na mwili wake kukutwa tarehe 13 Machi, 2024 kwenye msitu wa Jeshi karibu na Shule aliyikuwa anasoma.

 Mtoto huyo aliondoka nyumbani kwao na mtoto mwenzake tarehe 12 Machi 2024 majira ya 11:30 jioni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Polisi Kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Ufuatiliaji mkali unaendelea kumtafuta mtuhumiwa/ watuhumiwa waliohusika ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Imetolewa na Muliro J. MULIRO - SACP Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments