HEADLINES

6/recent/ticker-posts

POLISI DAR WAMDAKA MCHINA KISA KUTAPELI WATU MITANDAONI

Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao kimeendelea na kazi ya ufuatiliaji na kufanikiwa kwa mara nyingine kuwakamata Claudian Makaranga (28) mkazi wa Kawe, Kinondoni na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intanet nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.

Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.

Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebaika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Vifaa vilivyokamatwa ni Starline Dish 12, Starlink Router 12. Polisi Kanda Maalum ya Dar inatoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika. Pia amekamatwa Wilfred Werandumi (44) mkazi wa Tungi, Morogoro na Abdulrahim Mwakibinga (30), Mkazi wa Mwandege, Morogoro kwa tuhuma za kutumia majina ya Viongozi mbalimbali wa nchi kutapeli watu, kwa kujifanya wanaomba michango ya harusi, misiba na matibabu.

Baadhi viongozi ambao majina yao yametumika katika utapeli huu ni Mh. Dr. Stergomena Tax, Mhe. Innocent Bashungwa, Mhe. Mohamed Nchengerwa, Mhe. Eng. Hamadi Masauni, na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Daniel Chongolo. Amekamatwa pia Salum Kingu (25) mkazi wa Mbalizi, Mbeya na Loveness Silonga (24) mkazi wa Mbalizi, Mbeya kwa tuhuma za kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook yenye jina la KOPA FASTER TULIA TRUST FOUNDATION na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kutoka Ofisiya: - Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum, S.L.P.9140, DAR ES SALAAM …………… Simu: +255 (0) 22-2117705 Nukushi: +255(0) 22-2121 524 Baruapepe: utawala.dsmz@tpf.go.tz 23/01/2017 33 kwa watu mbalimbali kwa kudai kuwa wanatoa mikopo kwa masharti nafuu na haraka wakitumia namba ya simu 0749704445.

Jeshi la Polisi linaendelea na ufuatiliaji mkali wa tabia hizi na watuhumiwa wote watashughulikiwa vikali kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na ; Muliro J. MULIRO - SACP Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments