HEADLINES

6/recent/ticker-posts

POLISI KUONGEZA ULINZI KWA WAANDISHI ASKOFU MWAMAKULA ATIA NENO

Na Mwandishi Wetu,

DAR ES SALAAM

Askofu Emaus Mwamakula awapongeza klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaama na jeshi la polisi kwa kuwa na midahalo ya pamoja iliyofikia maazimio mbalimbali ya kujenga ushirikiano mzuri wenye tija sambamba na ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamejiri Machi 22,2024  hoteli ya CBD katika mdahalo wa majumuisho yaliyowakutasha baadhi ya  viongozi wa klabu ya waandishi, makamanda wa mikoa ya kipolisi, viongozi wa dini na wadau mbalimbali. 

Aidha, katika mdahalo huo imeundwa kamati ndogo kwa ajili ya kusimamia ulinzi na usalama wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Kamati hiyo yenye wajumbe sita imeundwa Machi 22, kwenye mdahalo wa majuisho kati ya DCPC na Jeshi la Polisi. 

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Malulu, ambaye pia ni RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Askofu Emaus Mwamakula na Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu.

Wengine ni Wakili Mkumbo Emmanuel, Katibu Mkuu wa DCPC, Fatuma Jalala na Bakari Kimwanga (mwanachama wa DCPC).

Kuundwa kwa Kamati hiyo ni matokeo ya midahalo mitatu kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari, lakini pia pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria. 

Midahalo hiyo iliyoanza Novemba 2023 na kumalizima Februari  2024, iliratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kudhaminiwa na shirika la IMS, ilihusisha Kanda Maalum (Ilala ikiwemo), Temeke na Kinondoni, ambapo maazimio kadhaa ya kiutendaji yalifikiwa.

Post a Comment

0 Comments