HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RAIS MWINYI ASHUKURU KWA DUA ZA HAYATI MZEE MWINYI


 Na Mwandishi,

ZANZIBAR.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema familia ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi imefarijika sana tangu alipofariki dunia kwa Dua zilizofanyika katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kumuombea.

Ameshukuru kwa Dua  zilizosomwa kumuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo katika kisomo cha Dua  ya Arubaini ya  Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja iftari iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja tarehe: 07 Aprili 2024.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema leo ni siku ya kipekee asubuhi imefanyika Hitma ya  kuombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na  jioni Hayati Ali Hassan Mwinyi. 

Dua hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyombo vya ulinzi na usalama, Dini , Vyama vya Siasa na Wananchi.


Post a Comment

0 Comments