HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RC CHALAMILA WALIOLIPWA FIDIA BONDE LA MSIMBAZI WASIENDE KUJENGA MABONDENI


Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wake  na waandishi wa habari Ofisini kwake Ilala Boma ambapo amesema bomoa bomoa inaendelea katika bonde la mto msimbazi ili kupisha uendelezaji wa kingo za mto msimbazi, na miundombinu mingine ya kisasa

Aidha RC Chalamila amesema kupitia uboreshaji wa mto msimbazi litapatikana eneo nzurii kwa ajili ya Shughuli za utalii na ujenzi wa hotel pembezoni mwa mto msimbazi hivyo wale wote ambao wameshalipwa fidia waende wakajenge katika maeneo mazuri wasiende tena kujenga mabondeni "ni vizuri kuchukua taadhari kwa kutojenga mabondeni kwa kuwa mvua bado zipo" Alisema RC Chalamila

Hata hivyo RC Chalamila amewataka viongozi wa Kata na mitaa kusimamia vema usafi katika maeneo yao ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.


Mwisho RC Chalamila ametangaza tarehe ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kwa Wilaya ya Kigamboni na Ilala kuanzia tarehe 19/04/2024.

Post a Comment

0 Comments