HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAKANUSHA KUSAJILI MAGROUP YA WHATS APP


Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

Serikali kupitia Msajili wa Jumuiya ya asasi za Kiraia imesema haisajili magroup ya WHATSAAP kama inavyoelezwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Akiongea na waandishi wa habari leo Aprili 3, 2024 jijini Dar es Salaam, Msajili wa Jumuiya za Kiraia Emmanuel Kihampa amesema katika maelezo yake aliyoyatoa kwenye mazungumzo yake ni kuwa kinachosajiliwa sio magroup ya Whatsaap bali ni vikundi vya Kiraia ama taasisi za Kiraia ambavyo vimekuwa vinajiendesha kupitia magroup ya Whatsaap kutokana na ukuwaji wa Teknolojia hivyo vikundi ama asasi hizo hujikuta zinafanya mambo yao kama mikutano na majadiliano yao kupitia Magroup ya Whatsapp Kihampa amesema sababu ya kunukuliwa kusajili magroup ya Whatsaap ni kutokana na kuwa vikundi vingi vya Kiraia vinajiendesha kupitia mtandao wa Whatsaap na kutokana na takwa la kisheria kuvitaka vikundi vyote vya kiraia ni lazima visajiliwe na sio magroup ya Whats App


Post a Comment

0 Comments