HEADLINES

6/recent/ticker-posts

AMO FOUNDATION, AMH YASHIKA MKONO WATOTO WENYE SARATANI MUHIMBILI


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Jamii imeaswa kujitokeza kusaidia wenye uhitaji wa katika nyanja mbalimbali ikiwemo wenye uhitaji wa huduma za afya.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kiongozi  wa Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  Sister Magdalena Kiula amesema wagonjwa tatizo la Watoto kupungukiwa damu “Hematology’ na Sokoseli limekua kubwa sana hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo na kuwaasa wazazi kuwapeleka hospitali kupata huduma na  kuacha kuamini ushirikina.

Kwa upande wao Wakurugenzi wa Taasisi za Amo Foundation na AMH Investment waliofika Hospitalini hapo kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika wodi ya wazazi kwa Watoto wenye matatizo ni wakati wa jamii kujitoa kwa matendo ya huruma katika kusaidia wahitaji.

Misaada iliyotolewa katika Wodi hiyo ni pamoja na sabuni, taulo za watoto, viatu, baiskeli mwendo nk.


Nyinginezo

Post a Comment

0 Comments