HEADLINES

6/recent/ticker-posts

ILI AFRIKA IENDELEE KUWA SHAMBA LAO BASI WATUSAIDIE-RAIS DKT.SAMIA SULUHU


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan leo katika uzinduzi wa  mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034  amesema kuwa Tarehe 14 Mei mwaka huu Tanzania itakua Mwenyekiti mwenza katika Mkutano wa nishati safi ya kupikia barani Afrika utakaofanyika  Jijini Paris Ufaransa na unatarajia kuhudhuriwa na watu 900wakiwemo wakuu wa nchi na Serikali, Taasisi za kifedha,  Washirika wa Maendeleo, Wanazuoni, Watekelezaji wa Nishati Jadidifu, Wadau wa sekta binafsi nk.

Masuala muhimu yatakayojadiliwa ni pamoja na ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia na masuala ya kisera na ushirikiano katika kusukuma ajenda ya nishati safi ya kupikia ambapo Rais Samia amesema katika Mkutano huo.

“Bara la Afrika tunakwenda kupaza sauti kwa mashirika ya fedha na wadau wao wanaowachangia kwenye mashirika ya fedha kupitia mizunguko mbalimbali wanayochanisha fedha kwa mfano kwa upande wa benki ya Dunia wana mzunguko wanaita IDA wana watu wao, wajumbe wao wanaowachangia benki ya Dunia tunakwenda kuwaomba waongeze michango wasirudi nyuma ili Afrika iendelee kuwa bara litakalotoa huduma ya bure kwa Ulimwengu kunyonya hewa ya Carbon kwenye misitu yetu lazima watuwezeshe tuelekee kwenye nishati safi ya kupikia”

Aidha Rais Dkt.Samia ameendelea kusema kuwa kuna majadiliano watakwenda nayo ya kuwa watu waache kutumia gesi lakini watumie gesi “Sisi Afrika tunakwenda kupaza sauti watuwezeshe tuendelee kutumia gesi kuelekea kwenye matumizi ya nishati nyingine tutakazokua tunajadiliana kila tunavyokwenda lakini kwa sasa Mungu ametubariki na gesi lazima watuwezeshe kutumia gesi ili tuipe nafuu sekta ya misitu ipumue na iweze kutoa huduma ya bure kwa Ulimwengu kuweza kunyonya hewa  ukaa inayotoka n ahii hewa ukaa sisi tunatoa asilimia tano tu  lakini nyingi inatoka huko kwao sisi tunawanyonyea huku, kwahiyo ili Afrika iendelee kuwa shamba lao basi watuchangie tuweke miundombinu na tuweke utaratibu wa kuweka nishati safi ya kupikia ili miti ipumue”

Rais Samia amesema kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ndani ya kipindi cha miaka 10 haitakuwa kazi rahisi lakini penye nia pana njia hivyo kwa kuwa wote tuna nia moja tutafikia azma ya malengo yetu kwa kila mdau atatumia kipawa na maarifa yake basi tutafika iyo 2034.

Vilevile Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kwa Wizara ya Nishati kuhakikisha inawafikishia wadau mkatati huu kwa njia rasmi na pia iuweke katika Tovuti na mitandao ya kijamii  ya wizara kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Agizo la pili alilowapa Wizara hiyo ni kukaa na wadau husika wa Serikalini na Sekta binafsi kubaini maeneo ambayo yakifanyiwa kazi yataongeza uharaka wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa bei nafuu ili wananchi wengi zaidi waweze kutumia akihimiz kushirikiana na sekta za fedha na mipango kufanikisha hilo.

Agizo la tatu ni kuwa na mfuko wa nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2025 akiwaagiza kuja na sheria itakayowezesha kupatikana kwa mfuko huu, la nne ni TAMISEMI iboreshe mikataba wanayoingia na Wakuu wa Mikoa na Wilaya ili kuongeza kifungu cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye upimaji wa utendji kazi wao.


Post a Comment

0 Comments