HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATAKA WIZARA YA NISHATI KUTAFUTA WABUNIFU TEKNOLOJIA KUFANIKISHA MPANGO WA KUWAWEZESHA WATUMIAJI WA GESI KULIPIA KADRI WANAVYOTUMIA

Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Nishati kutafuta Watanzania Wabunifu wa teknolojia na kuwapa kazi ya kufanikisha mpango wa kuwawezesha Watumiaji wa gesi ya kupikia wawe wanalipia kadri wanavyotumia kama inavyofanyika kwenye LUKU za umeme.

Akiongea leo wakati akiuzindua Mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia wa mwaka 2024 Jijini Dar es salaam, Rais Samia amenukuliwa akisema yafuatayo “Serikali tunalo jukumu la kuongeza uelewa kwa Wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia na kutunga sera nzuri na wezeshi ili kufikia malengo ya mkakati huu, katika hili wenzetu wa Wizara ya Nishati watatuongoza kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa uhakika na kwa bei inayohimilika kwa Wananchi”
“Sekta binafsi tunaitarajia pamoja na kuongeza uwekezaji na kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia sehemu mbalimbali Nchini watuletee pia teknolojia rahisi itakayowezesha Wananchi kupata nishati safi kadri ya uwezo wao kwa mfano kulipia kadri anavyotumia kama inavyofanyika kwa umeme na maji, zile pre paid meters”
“Na hapa nataka niseme Waziri kwamba moja kati ya maonesho ya mazingira niliyowahi kutembelea nishaikuta hii teknolojia kuna Watanzania wametengeneza mitungi ambayo unatumia gesi jinsi unavyolipa, unachukua mtungi mzima kama umelipa elfu 10 utatumia gesi yako ya elfu 10 ikimalizika mtungi unakata hata kama gesi ipo mpaka uwasiliano nao tena ulipe tena wakufungulie utumie tena naomba sana watafute au kama wapo wajitokeze tufanye nao kazi katika eneo hili” - Rais Samia.


Post a Comment

0 Comments