HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TRA TAASISI YA KWANZA KUTAMBUA MCHANGO WA WANAHABARI WA MITANDAONI


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi na mawasiliano wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga amesema akama mamlaka ya mapato kwa niaba ya Kamishna mkuu watakua bega kwa bega na waandishi wa Habari wa Mitandaoni kupitia Jukwaa hilo JUMIKITA Lililo chini ya Mwenyekiti wake Shabani Matwebe.

Kamoga amesema “Nikuahidi wewe pamoja na jukwaa zima la wanahabari wa mitandao sisi tutakua bega kwa bega na ninyi na tutafanya kazi na ninyi, tutaendelea katika kufanya kazi na ninaamini Forum hii haitakua ya kwanza tumeanza naona ni mwanzo mzuri lakini ninaamini tutaenda ten ana tena, mkiwa na jambo na mkihitaji nafasi yetu ushiriki wetu tutapanga tuone”.

 


Tutaona ni kwa namna gani wezeshwaji huu ufike hadi mikoani tuwe na Forum za wanahabari wa mitandaoni kwenye kanda zetu au mikoani naamini kwenye mwezi wa 11 au wa 12 tutafanya pamoja”

 Kamonga amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Semina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni JUMIKITA.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe amesema ni wakati sasa kwa waandishi wa Habari wa mitandaoni kwani kwa sasa dunia ya  ‘Digital Platform’ haikwepeki hivyo anatambua na kuonaTRA kuwa Taasisi ya kwanza kutambua mchango wa waandishi wa Habari wa Mitandaoni.

“Digital Platform ni dunia haikwepeki unaweza kuwa na ‘Followers’ (wafatiliaji) elfu 50 lakini ukiweka Tangazao likaonekana na watu zaidi ya hao. Ikitokea mtu amewatambua, amejua ukubwa wenu lazima tumpongeze.

 Semina hiyo ya siku moja imefanyika katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi wa mitandaoni kutoka katika vituo mbalimbali.





 


Post a Comment

0 Comments