HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WANAHABARI KUONGEZA MKAZO UPOTOSHAJI MITANDAONI SERIKALI KUTOA USHIRIKIANO


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wanahabari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania Elizabeth Riziki amesema mwaka huu wamelenga kuangalia uchechemuzi wa Uhuru wa kujieleza hasa tunapoelekea katika Chaguzi 2 kubwa hapa nchini ikiwemo wa Serikali za Mita ana Uchaguzi Mkuu.

Amesema wanaangalia ni kwa namna gani Asasi za kiraia na Waandishi wa habari wanaweza kushirikiana kuhakikisha elimu ya ushiriki katika Uchaguzi inawafikia jamii.

“Tukitaka kuangalia uhuru wa habari au uhuru wa kujieleza lazima tukumbuke kitu cha msingi ambacho kinatulinda Taifa tulilonalo nafasi tuliyonayo sifa tuliyonayo kama Watanzania ni pamoja na urithi tulioupokea kutoka kwa wazee wetu ambao una maadili namiongozo Fulani, hivyo tutaendeleza uchechemuzi huu kwa kuzingatia maadili ya kitanzania, Seria zinazotuongoza lakini ni Rai yetu kuwaambia wanahabari na wadau wa maendeleo kuendelea kufanyia kazi hasa katika eneo la mtandao.

"Intaneti AI vimekuja kwetu kwa fujo kitu ambacho kinatufanya sisi tuwe makini sana nama gani tunapata taarifa na tunazihakiki vipi ni Rai kwetu tunaahidi kutafuta suluhu au mwarobaini wa kumaliza hili tatizo”

 

Elizabeth Riziki amesema hayo leo Mei 32-2024 wakati wa Jukwaa la uwajiikaji kwa Wanahabari katika kutambua majukumu yao hususan katika Uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza na ushiriki wa wanahabari katika kuelewesha jamii katika kushiriki Uchaguzi.

Kwa upande wake Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi amesema serikali itakua mstari wa mbele katika kushirikiana na Wanahabari.

“Sera ya habari ya mwaka 2003 inafanyiwa mapitio mwaka huu tutakamilisha na tutakuwa na sera nyingine itakayosimamia sekta ya  uandishi na utangazaji, mchakato unaofanyika sasa ni kutathmini mafanikio, changamoto na kutoa mapendekezo sera iwe ni ya namna gani lengo likiwa ni kuoneza uhuru wa habari, hatujafika tunapokwenda lakini tumeshaondoka mahali tulipokuwa na tunasafiri hatua kwa hatua”

Aidha Matinyi amewataka wanahabari kuzinagtia sheria, kanuni na taratibu wakati wa majukumu yao na serikali wajibu wao ni kulinda na kumhudumia kila raia.





Post a Comment

0 Comments