HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MTIA NIA URAIS IFM AITAKA SERIKALI KUTOINGIZA SIASA VYUONI


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Mtia nia wa nafasi ya Urais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM kilichopo Jijini Dar es Salaam Barnabas Samwel amesema kumekuwa na changamoto kutoka kwa baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi na familia zao kuingiza siasa katika maslahi ya wanafunzi.

“Kwa bahati mbaya kumekuwa na baadhi ya watu kukandamiza wanafunzi wamekua wakileta ukandamizaji na skendo mbalimbali za kwamba huyu kuna maelekezo kutoka juu basi atakatwa mimi kinachonishangaza ni kwamba je kunakua na maelekezo gani tena kutoka juu na hayo maelekezo yanatoka wapi na wakati Katiba TCU Regulations Act na IFMSO Constitution inakataa yoyote kujihusisha na masuala ya siasa” amesema Barbabas.

Barbabas ameitaka Serikali kufuata Sheria na kanuni zinazozuia wanafunzi kujihusisha na masuala ya siasa.

Aidha katika hatua nyingine  amesema atasaidia kuondoa dhana kandamizi  iliyojengeka kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopewa haki moja ya kupiga kura kwa viongozi wa juu kwa kutogombea nafasi za uongozi kuwa na sifa ya kugombea na kupigiwa kura za nafasi za juu ikiwemo Urais.

Mbali na Barnaba anayetaka nafasi ya Urais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo hicho Amembatana na  Mike Diakite ambaye ni Mtia nia mweza wa nafasi ya Urais katika kurudisha fomu ya nafasi hiyo ambapo uchaguzi unatarajia kufanyika Juni 9 mwezi huu.

Post a Comment

0 Comments