HEADLINES

6/recent/ticker-posts

DARAJA LA SIMIYU NA SUKUMA KUKAMILIKA MWAKANI

Na Mwandishi Wetu,
MWANZA.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi.Godfrey Kasekenya amemtaka Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) anaejenga daraja la Simiyu lenye urefu wa mita 150 na Barabara   unganishi KM 3 na Mkandarasi Mumangi Construction Co. Ltd anayejenga daraja la Sukuma kuongeza  kasi ya ujenzi wa madaraja hayo ili yakamilike mapema mwakani.
Muonekano wa daraja la sasa la Simiyu wilayani Magu mkoani Mwanza

Ameongea hayo leo wakati akikagua ujenzi wa madaraja hayo Mkoani Mwanza Wilayani Magu na kusisitiza umuhimu wa madaraja hayo kwa uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa.

"Hakuna sababu ya kuchelewesha ujenzi wa miradi hii kwani wakandarasi  wote wanauwezo mkubwa hivyo TANROADS wasimamieni kikamilifu ili tupate thamani ya fedha", amasema Eng. Kasekenya. 

Kazi ya ujenzi wa nguzo za daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 ikiendelea.

Naibu Waziri Kasekenya amesema madaraja hayo  ya kimkakati  yatafungua fursa za kiuchumi hivyo kuwataka wananchi kuongeza tija ya uzalishaji ili kukuza biashara na nchi jirani.

   Mhandisi. Kasekenya amezungumzia umuhimu wa wananchi wanaoishi jirani na miradi hiyo kuelimishwa namna ya kunufaika na fursa za ujenzi wa miradi hiyo ili kupata ajira na kuilinda ili idumu kwa muda mrefu.


Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amekagua ujenzi wa barabara ya Isandula Hungumalwa KM 10 inayojengwa kwa lami.

Imetolewa na KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI

Post a Comment

0 Comments