HEADLINES

6/recent/ticker-posts

POLISI WATIA KOROKORONI WASHUKIWA WANNE WALIOFANYA UBAKAJI WA BINTI


Na Mwandishi Wetu,
DODOMA.

Polisi Tanzania limewakamata Watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu wa kumbaka na kumlawiti Msichana na kusambaza video yake mitandaoni ambapo imebainika tukio lilifanyika Swaswa Dodoma mwezi May 2024.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa leo August 09,2024 imesema

 “Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson”

“Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe Mahakamani,

kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani” 

Aidha Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya uchunguzi wa tukio ambalo lilisambazwa katika mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo (video clip) kuanzia August 2, 2024 ikimwonyesha Msichana mmoja akifanyiwa vitendo vya ukatili ambapo uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata Msichana na amehifadhiwa eneo salama akipata huduma zinazostahili kupewa Mtu aliyefanyiwa ukatili wa aina hiyo.

Polisi wamesema uchunguzi umebaini kuwa tukio hilo lilifanyikia eneo la Swaswa katika Jiji la Dodoma mwezi May 2024.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa leo August 09,2024 imesema

 “Watuhumiwa wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza taarifa za ongo mitandaoni zinazosema RIP Binti aliyebakwa na kulawitiwa akutwa amefariki”
“Taarifa nyingine ya uongo inasema Mama wa binti huyo amedondoka na kufariki Watuhumia wawili wamekamata huko Arusha na wawili Mkoani Dar es salaam ambao majina yao ni Amos Lwiza, Adam Dongo, Venance Mallya na Isack Elias


Imetolewa na David Misime

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Dodoma, Tanzania. 

Post a Comment

0 Comments